SOKA: Manchester United yaizamisha Brighton
2021-04-06 16:22:53| cri

Mason Greenwood alijitokeza wakati mwafaka zaidi kuisaidia Manchester United kubeba ushindi kwa kuifunga Brighton 2-1 ugani Old Trafford usiku wa Jumapili. Bao la mapema la Brighton lilifungwa na Danny Welbeck kabla ya Marcus Rashford kusawazishia wenyeji katika kipindi cha pili. Brighton walitaka kupewa penalti baada ya Harry Maguire kuonekana kumchezea rafu Welbeck, lakini refa Mike Dean ambaye alikuwa anasimamia mchezo huo alipuuza. Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer walifaulu kuzoa alama zote tatu, na hivyo kuhifadhi nafasi yao ya pili wakiwa wamesalia na mechi nane kukamilisha msimu huu.