SOKA: Kocha Gomez afichua siri ya mafanikio Simba SC
2021-04-07 16:11:39| cri

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Didier Gomes Da Rosa amewapongeza wachezaji wake kwa kutekeleza maelekezo anayowapa katika michezo ya ushindani na wanapokuwa mazoezini. Gomez ametoa pongezo hizo, huku kikosi chake kikiwa safarini kuelekea nchini Misri, tayari kwa mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Makundi dhidi ya Al Ahly, utakaochezwa Ijumaa. Amesema nidhamu ya kufuata maelekezo kwa wachezji wake imekua njia sahihi iliyowafikisha kwenye furaha ya kutinga hatua ya Robo Fainali, wakiwa na mchezo mmoja mkononi.