Watu 15 wafariki nchini Kenya katika ajali ya barabarani
2021-04-07 18:11:48| Cri

Watu 15 wafariki nchini Kenya katika ajali ya barabarani_fororder_VCG111324672067

Watu 15 wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa mapema leo baada ya mabasi mawili ya abiria kugongana uso kwa uso katika mji wa pwani wa Malindi, nchini Kenya.

Mkuu wa Kaunti ya Kilifi, Kutswa Olaka amesema, madereva wa mabasi hayo, moja likitokea Mombasa kuelekea Garissa, na lingine likielekea Mombasa, walifariki katika ajali hiyo iliyotokea kwenye barabara kuu ya Malindi – Mombasa.

Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema, dereva wa basi lililokuwa likielekea Garissa alishindwa kulidhibiti gari wakati alipojaribu kupita gari lingine, na kugonga basi lililokuwa likielekea Mombasa.