UM wahimiza vyama vya Sudan Kusini kuharakisha utekelezaji wa majukumu ya amani
2021-04-07 09:08:33| CRI

 

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini David Shearer amezihimiza pande zote za makubaliano ya amani ya mwaka 2018 nchini Sudan Kusini kuharakisha utekelezaji wa majukumu ya kufikia amani na utulivu kabla ya uchaguzi utakaofanyika mwaka 2023.

David amesema ingawa pande hizo zimepiga hatua tangu kuanzishwa kwa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa Februari mwaka jana, lakini mchakato wa amani bado ni dhaifu.