BASKETBALL: Doncic na Holiday wachezaji bora NBA wiki ya 15
2021-04-07 16:10:23| cri

Mcheza kikapu wa timu ya Dallas Mavericks, Luka Doncic amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa wiki ya 15 kwenye ligi kuu ya kikapu nchini Marekani (NBA) kwa upande wa Magharibi baada ya kuonesha kiwango safi kilichoifanya timu yake kushinda michezo mitano mfululizo. Jrue Holiday wa timu ya Milwaukee Bucks amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo wa wiki ya 15 kwa upande wa Mashariki baada ya kufikisha wastani wa alama 26.8, rebaundi 8.5 na wastani 62.7 wa kufunga mabao uwanjani na kusaidia timu yake kushinda michezo mitatu.