Nigeria yatangaza hali ya hatari katika magereza baada ya shambulizi
2021-04-07 18:11:25| Cri

Magereza nchini Nigeria zimewekwa kwenye hali ya tahadhari baada ya shambulizi dhidi ya makao makuu ya polisi na gereza lililoko mkoa wa Imo, kusini mwa nchi hiyo.

Makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo amesema, mfumo wa usalama nchini humo utafanyiwa marekebisho, na kuhakikisha kuwa serikali kuu itaimarisha ulinzi katika magereza yote nchini Nigeria.

Makamu huyo wa rais amelaani shambulizi hilo, na kusema kuwa wahusika wote watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.