Kampuni ya Huawei yapanua huduma za 4G kaskazini magharibi mwa Ethiopia
2021-04-07 09:06:41| CRI

 

 

Kampuni ya mawasiliano ya China, Huawei, imetangaza kuwa imepanua huduma za kizazi cha nne (4G) cha teknolojia ya huduma za simu katika miji minne mikubwa iliyoko kaskazini magharibi mwa Ethiopia.

Katika taarifa ambayo Shirika la Habari la China Xinhua imeipata, Huawei imesema imeingia ubia na Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Ethiopia ili kupanua huduma ya 4G katika miji mingi zaidi ya kaskazini magharibi mwa Ethiopia, ikiwemo Bahir Dar, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Amhara.

Kwa zaidi ya miongo miwili, kampuni ya Huawei imejihusisha na maendeleo ya Ethiopia, ambapo mpaka sasa imetoa nafasi zaidi ya 300 za ajira, na kunufaisha watu zaidi ya milioni 45 kwa huduma na bidhaa zake.