SOKA: TFF yafafanua adhabu ya Mwakalebela
2021-04-07 16:10:49| cri

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefafanua kuwa adhabu aliyopewa makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kuwa imeegemea kwenye uapnde wake wa uongozi wa klabu na si kwenye masuala mengine ya kama vile kumzuia asifuatilie taarifa za michezo. Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema hayo alipojibu malalamiko ya makamu mwenyekiti huyo, ambaye siku tatu zilizopita alisema amezuiwa asisome magazeti ya michezo wala kutazama luninga.