Rais wa China azitaka Ujerumani na Umoja wa Ulaya kushirikiana na China kuleta utulivu duniani
2021-04-07 19:58:36| Cri

Rais wa China Xi Jinping leo amezitaka Ujerumani na Umoja wa Ulaya kufanya juhudi za pamoja na China ili kulinda na kuboresha maendeleo ya utulivu ya ushirikiano wao, na kuleta uhakika zaidi na utulivu duniani.

Katika mazungumzo yake kwa simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Rais Xi amesisitiza kuwa yeye na Bi. Merkel wamewasiliana mara kadhaa mwaka jana, jambo lililochukua nafasi kubwa ya uongozi katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ujerumani na China na Umoja wa Ulaya.