SOKA: AFC: Wasiwasi waibuka kambi ya AFC Leopards kufuatia Kocha Aussems kuondoka nchini Kenya
2021-04-07 16:11:17| cri

Klabu ya AFC Leopards ya nchini Kenya imekumbwa na wasiwasi baada ya kocha Patrick Aussems kuondoka nchini humo, kufuatia marufuku ya serikali iliyositisha tena michezo ili kudhibiti wimbi la tatu la virusi vya Corona. Mbelgiji huyo aliondoka baada ya Rais Uhuru Kenyattta kutangaza marufuku hayo kwa muda wa siku 21. Aussems ni miongoni mwa makocha walioamua kurudi nyumbani ili kuwa karibu na familia zao wakati ambapo marufuku inatekelezwa.