Watu 50 wauawa katika mapambano yaliyotokea Darfur ya Magharibi, Sudan
2021-04-07 09:08:04| CRI

 

 

Kamati ya Madaktari nchini Sudan imesema mapambano yaliyotokea katika jimbo la Darfur Magharibi nchini humo yamesababisha vifo vya watu 50 na wengine 132 kujeruhiwa.

Wakati huo huo, Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan imesema, watu 56 wameuawa katika mapambano kati ya makabila ya Masalit na Kiarabu huko El Geneina, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Magharibi.

Baraza la Usalama na Ulinzi la Sudan limetangaza hali ya hatari katika Jimbo la Darfur Magharibi na kupeleka vikosi vya usalama kwa lengo la kumaliza mapambano hayo.