Iran yathibitisha kutokea kwa mlipuko katika meli yake ya kibiashara iliyoko katika Bahari Nyekundu
2021-04-07 19:31:31| Cri

Iran yathibitisha kutokea kwa mlipuko katika meli yake ya kibiashara iliyoko katika Bahari Nyekundu_fororder_VCG111324670704

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imethibitisha kutokea kwa mlipuko katika meli ya kibiashara ya nchi hiyo, Saviz, katika Bahari Nyekundu karibu na pwani ya Djibouti Jumanne.

Shirika la Habari la Wanafunzi la Iran limemnukuu msemaji wa Wizara hiyo Saeed Khatibzadeh akisema, meli hiyo imeharibika kidogo kutokana na mlipuko huo, na kuongeza kuwa, hakuna taarifa zozote za vifo au majeruhi zilizoripotiwa katika ajali hiyo.

Amesema meli hiyo ya kiraia iliwekwa katika Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden kutoa usalama wa baharini katika njia za meli na kupambana na maharamia.

Khatibzadeh amesema, chanzo cha mlipuko huo bado kinachunguzwa, na Iran itachukua hatua zote za lazima kupitia taasisi za kimataifa katika kutimiza hilo.