IMF yaongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia kufikia asilimia 6
2021-04-07 09:06:03| CRI

 

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetoa makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia, na kusema utakua kwa asilimia 6 kwa mwaka 2021, ikiwa ni alama 0.5 zaidi ya makadirio yaliyotolewa mwezi Januari.

Katika ripoti ya hivi karibuni ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia, Mchumi Mkuu wa IMF Gita Gopinath amesema, inatarajiwa kuwa hatua ya kufuatia mamilioni ya watu kupata chanjo ya virusi vya Corona itaongeza nguvu ya kufufuka kwa uchumi wa nchi mbalimbali baadaye mwaka huu. Amesema mataifa pia yanaendelea kubuni njia mpya za kufanya kazi licha ya kupungua kwa safari, na nchi kubwa kiuchumi, hususan Marekani, kutoa fedha zaidi za kusaidia kukabiliana na athari za virusi hivyo.

Ripoti hiyo pia imesema, kati ya nchi zinazoibuka na zinazoendelea, uchjumi wa China unakadiriwa kukua kwa asilimia 8.4 mwaka huu, ikiwa ni alama 0.3 zaidi ya makadirio yaliyotolewa Januari.