Kuondoa umaskini uliokithiri nchini China ni utekelezaji mzuri zaidi wa haki za binadamu
2021-04-07 08:46:05| CRI

Serikali ya China imetoa kijitabu cheupe kuhusu utekelezaji wa China katika kazi ya kupunguza umakini ya binadamu, kikitumia takwimu halisi na mifano mbalimbali kukumbusha mafanikio yaliyopatikana na Chama cha Kikomunisiti cha China CPC kikiwaongoza wachina katia vita dhidi ya umaskini na kujumuisha uzoefu bora wa China katika kupunguza umaskini. Kijitabu hicho kimethibitisha tena mtazamo wa baadhi ya wachambuzi kwamba China kuondoa umaskini uliokithiri sio tu ni mradi mkubwa zaidi wa haki za binadamu duniani, bali pia ni utekelezaji mzuri zaidi wa haki za binadamu.

Kwa kufuata vigezo vinavyokuwepo hivi sasa, watu milioni 98.99 maskini wa vijijini wameondokana na umaskini, wilaya 832 maskini zimefanikiwa kuondoa umaskini, huku vijiji elfu 128 vimeondolewa kutoka orodha ya umaskini. Rais Xi Jinping wa China mwishoni mwa mwezi wa Februari ametangaza ushindi wa China katika vita dhidi ya umaskini, ambao umeleta ufuatiliaji wa dunia nzima. Watu wengi wameshangazwa na miujiza ya China katika kupunguza umaskini, na kutana kujua jibu la “kwa nini China inaweza kupata mafanikio makubwa namna hiyo”.

Kijitabu hiki kimetungwa juu ya msingi wa utekelezaji wa China katika kupunguza umaskini, na kujumuisha mfululizo wa uzoefu wa kupunguza umaskini, ambao ni pamoja na kuweka umma katika kiini cha maendeleo, kuweka kipaumbele umaskini katika utawala, kuondokana na umaskini kwa njia ya maendeleo, kuhimiza mchakato wa kupunguza umaskini kwa kulingana na hali halisi, kutoa mchango wa kundi la watu maskini, kuunganisha nguvu za pande mbalimbali. Lakini kinacho kuwa muhimu zaidi ni kwamba siku zote chama tawala cha China kinachukulia umma kama kiini katika kazi ya kusaidia na kupunguza umaskini.