TCCIA Arusha waweka juhudi za kuvutia watalii
2021-04-07 18:31:33| cri

Chama cha wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) na Halmashauri ya Jiji la Arusha, wameanzisha mpango wa pamoja wa kupanda miti ili kuboresha zaidi mandhari ya jiji hilo na kutengeneza vivutio vipya vya utalii vitakavyosaidia kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii.

Ofisa Mtendaji wa TCCIA mkoani Arusha, Charles Makoi, amesema mpango huo wa ushirikiano, unalenga kuotesha miti 20,000 kwa mwaka huu.

Hadi kufikia sasa wamefanikiwa kuotesha miti 100 katika bustani tengefu ya Mto. TCCIA imesema imeamua kuwekeza katika masuala ya utunzaji wa mazingira ili kuiboresha zaidi sekta ya utalii na masoko katikati ya Jiji la Arusha.

Makoi amesema mpango huo ulianza rasmi mwaka uliopita, kwa kupanda miti 20,000 katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame ikiwemo miji ya Muriet na Morombo.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), pia imekuwa ikihamasisha uboreshaji wa miradi ya mazingira ya biashara na uwekezaji, kwa njia ya majadiliano ili kuwainua wananchi kiuchumi.