China yasema kasi ya mchakato wa kisiasa nchini Mali inapaswa kudumishwa
2021-04-07 09:07:08| CRI

 

 

Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa, Dai Bing amesema, kasi ya mchakato wa kisiasa nchini Mali unapaswa kudumishwa. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja huo, Balozi Dai amesema hali ya jumla nchini Mali inaendelea kuwa nzuri, na wakati huohuo, nchi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ugaidi, virusi vya Corona na mgogoro wa kibinadamu.

Amesema serikali ya Mali imeandaa mpango wa mpito, na utekelezaji wake ni jukumu kubwa linalofuata, na kuongeza kuwa, wakati serikali hiyo inapofanya uratibu na kuendelea na maandalizi ya uchaguzi, juhudi chanya pia zitasaidia kuimarisha maendeleo, na kuboresha maisha ya watu katika njia ambayo inaweza kuleta manufaa zaidi kwa wananchi wake.