Wataalam wa Afrika wahimiza kujumuisha nishati barani humo
2021-04-07 09:09:00| CRI

 

 

Wataalam kutoka vyuo vikuu na Umoja wa Afrika wamesema, nchi za Afrika zinahitaji kujumuisha nishati zao kwa maendeleo endelevu ya uchumi na kufufua uchumi baada ya janga la COVID-19.

Wataalam hao wamesema, nishati, ni pembejeo muhimu ya kiuchumi na kijamii, katika kutimiza maendeleo endelevu ya bara la Afrika, kama ilivyopendekezwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.