Tanzania kuunda timu ya kutathmini maambukizi ya COVID-19 nchini humo
2021-04-07 09:09:29| CRI

 

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, anapanga kuunda timu maalumu ya wataalam ili kutathmini maambukizi ya COVID-19 nchini humo. Amesema timu hiyo itapendekeza na kuwezesha serikali kufanya maamuzi, na pia itatathmini athari za janga la COVID-19 kwa sekta ya utalii. Amesistiza kuwa Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa wakati wa kukabiliana na janga hilo.