Mastercard yanunua hisa kwa kampuni ya Airtel Afrika
2021-04-07 18:30:18| cri

Mastercard Kampuni ya Mastercard ambayo inaongoza kwenye teknolojia yaufanyaji malipo imenunua hisa za dola milioni 100 katika biashara za fedha kwa njia ya simu kwenye kampuni ya mawasiliano ya simu ya Airtel barani Afrika. Kwenye taarifa yake, Mastercard imesema itachukua asilimia kidogo ya biashara ya fedha ya kampuni hiyo ya Airtel.  Katibu mkuu mtendaji wa kampuni ya Airtel Afrika Bw Raghunath Mandava ameikaribisha Mastercard kama mwekezaji kwenye biashara hiyo ya fedha kwa kutumia simu.Machi mwaka huu, Airtel Africa ilitangaza uwekezaji mwingine wa dola milioni 200 kwenye biashara ya fedha kwa simu.  Amesema lengo kuu ni kuongeza mtaji utakaofanikisha huduma za mtandao, kuongeza mauzo na kulipa madeni ya kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu.