China yaorodhesha mapungufu matano ya Marekani katika kushughulikia haki za binadamu
2021-04-07 19:15:09| CRI

China yaorodhesha mapungufu matano ya Marekani katika kushughulikia haki za binadamu_fororder_VCG111322240284

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China imesisitiza mara kwa mara kuwa kauli ya “mauaji ya kimbari” haina ukweli wowote.

Amesema Marekani inapotoa taarifa zisizo za kweli kuhusu haki za binadamu nchini China na kujifanya kuwa mlinzi wa haki za binadamu, ni ishara kuwa haina imani na hali yake ya haki za binadamu, na inachafua nchi nyingine ili kuondoa ufuatiliaji wa watu kuhusu hali yake.

Amesema historia na hali halisi zimerekodi makosa ya Marekani ya kukiuka haki za binadamu, ukoloni, ubaguzi wa rangi, kuchochea vurugu katika nchi nyingine, kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kutumia vigezo viwili kati yake na nchi nyingine.

Amesisitiza kuwa, kwa muda mrefu Marekani imejitetea kuwa mfano wa kuigwa wa haki za binadamu, lakini pia imetumia vigezo viwili katika suala hilo, na kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine.