Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kongo yamthibitisha Bw. Denis Sassou Nguesso kuwa rais mpya
2021-04-07 17:24:23| cri

Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kongo imeidhinisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kuwa halali, na kuthibitisha rais wa sasa Bw. Denis Sassou Nguesso amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.

Mahakama hiyo imetangaza kuwa, Bw. Nguesso amepata asilimia 88.4 ya kura kwenye uchaguzi huo uliofanyika tarehe 21, mwezi uliopita.

Habari zinasema, rais Sassou Nguesso aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1979.