Tunisia na China zasaini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi
2021-04-07 09:07:38| CRI

 

 

Tunisia na China zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia yaliyoko mji mkuu wa Tunisia, Tunis.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Othman Jerandi amesema, makubaliano hayo mapya na China yataiwezesha Tunisia kunufaika na misaada ya kifedha kutoka China ambayo itasaidia katika maendeleo ya nchi hiyo. amesema, kwa mara nyingine tena, makubaliano hayo yameonyesha mshikamano na uhusiano imara kati ya Tunisia na China.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tunisia, Zhang Jianguo amesema, makubaliano hayo yanaonyesha uaminifu na ubora wa urafiki kati ya watu na nchi hizo mbili. Amesema baadhi ya miradi inayotekelezwa kwa msaada wa China nchini Tunisia imekuwa alama ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, ukiwemo mrasi wa Kituo cha Michezo cha Ben Arous.