Makamu wa rais wa China apongeza makamu mpya wa Tanzania
2021-04-07 20:24:26| CRI

Makamu wa rais wa China apongeza makamu mpya wa Tanzania_fororder_VCG111323646664

Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan leo ametoa barua ya pongezi kwa makamu mpya wa Tanzania Philip Mpango.

Bw. Wang Qishan amesema kuwa, China na Tanzania zina urafiki mkubwa, hali ya kuaminiana ya kisiasa ni thabiti, ushirikiano katika pande mbalimbali umepata matokeo makubwa.

Amesema anapenda kushirikiana na Bw. Mpango kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kunufaishana katika pande zote kuendelezwa siku hadi siku.