Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kujifunza kutoka mauaji ya Rwanda
2021-04-08 17:01:06| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kujifunza kutoka mauaji ya Rwanda_fororder_卢旺达大屠杀

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kwa pamoja kupambana na vitendo vinavyotokana na chuki ili kuzuia historia kujirudia.

Bw. Guterres amesema hayo katika Kumbukumbu ya miaka 27 ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, na kusema hivi sasa, makundi yenye msimamo mkali ambayo ni tishio kubwa kwa usalama wa nchi mbalimbali duniani.

Amesema tangu kutokea kwa janga la COVID-19, hali ya ubaguzi na ukosefu wa usawa kwenye jamii imezorota zaidi, jambo linalosababisha mapambano ya kimabavu.

Bw. Guterres ametoa wito kwa pande zote kuahidi kwa pamoja kujenga dunia inayowezesha kila mmoja awe na haki na heshima.