SOKA: Kevin de Bruyne asaini upya Man City
2021-04-08 18:27:54| cri

Kiungo wa Vinara wa Ligi Kuu ya England Manchester City, Kevin de Bruyne amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo inaendelea kuwa tishio ndani na nje ya England. De Bruyne ambaye alijiunga na Manchester City mwaka 2015 akitokea VfL Wolfsburg ya Ujerumani, amesaini mkataba mpya ambao utafikia kikomo mwaka 2025. Mkataba wa awali wa De Bruyne mwenye umri wa miaka 29 ulikua unafikia kikomo mwaka 2023.