WHO yasema kukabiliana ukosefu wa usawa katika sekta ya afya ni muhimu kwa Afrika baada ya janga la COVID-19
2021-04-08 10:22:37| cri

 

 

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, Bi. Matshidiso Moeti amesema, kutimiza ujumuishi na kasi ya ukuaji baada ya janga la virusi vya Corona barani Afrika kunategemea hatua za kivitendo zinazowajibika na matokeo ya mfumo dhaifu wa afya katika bara hilo.

Akizungumza katika Siku ya Afya Duniani iliyoadhimishwa jana jumatano, Bi. Moeti amesema janga hilo limevuruga zaidi ukosefu wa usawa katika sekta ya afya barabi Afrika, huku watu masikini wakikosa dawa muhimu za kuokoa maisha na kukinga ujauzito.

Amesema kaulimbiu ya Siku ya Afya mwaka huu ni “Kujenga Dunia ya Usawa na Afya” inasisitiza haja ya kukabiliana na vikwazo vya kifedha na kisera ambavyo vimezuia upatikanaji wa huduma bora za afya barani Afrika.

Ameongeza kuwa, unyanyapaa unaotokana na jinsia, kipato, umri, kiwango cha elimu, ukabila na ulemavu vimechochea ukosefu wa usawa wa huduma za afya barani Afrika.