UNHCR yatoa wito wa wakimbizi kupata chanjo ya COVID-19 kwa usawa
2021-04-08 10:23:55| cri

 

 

Jana, Aprili 7 ilikuwa ni Siku ya Afya Duniani. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetaka hatua za umoja na mshikamano wa kimataifa, ili kuhakikisha wakimbizi, watu waliolazimishwa kuhama na wale wasio na uraia wanapata chanjo ya COVID-19 kwa usawa.

UNHCR imesema hadi sasa ni nchi 20 tu ambazo zimetoa chanjo kwa wakimbizi kwa "usawa" kama raia wao, ikiwa ni pamoja na Serbia, Nepal, Rwanda na Jordan.