Jeshi la Somalia ladhibiti kambi za kundi la al-Shabab
2021-04-08 10:24:30| cri

 

 

Jeshi la Somalia (SNA) limesema limedhibiti kambi kadhaa za kundi la al-Shabab huko Galgaduud, katikati mwa Somalia katika operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi hilo. Kamanda wa jeshi hilo Mohamed Tahlil Bihi amesema, vikosi vya usalama viliteka kambi mpya katika maeneo ambayo ni ngome za al-Shabab na kusababisha vifo na majeruhi mengi ya kundi hilo. Operesheni hiyo imefanywa baada ya jeshi hilo kukomboa maeneo ya Sinadhaqqo na Labi Dulle wiki iliyopita huko Galgaduud ambapo magaidi wengi waliuawa na silaha zilikamatwa.