Serikali na taasisi za benki Tanzania kuwapiga jeki wakulima wa korosho
2021-04-08 17:09:55| cri

Serikali ya Tanzania imekutana na taasisi za kibenki na kukubaliana nazo kufungua akaunti ya pamoja kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa korosho ili kuinua kilimo cha zao hilo.

Makubaliano hayo yalifanyika jana jijini Dodoma ,kati ya Naibu Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe na wawakilishi wa mabenki hayo huku lengo likiwa ni kuwawezesha pia wakulima kupata pembejeo kwa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari,Bashe alisema amefanya kikao na benki ya Equity ambayo imeonesha nia yake ya kuwainua wakulima huku akiongeza kuwa benki zengine ambazo zimeonesha nia hiyo na kukubaliana ni pamoja na benki ya NMB na CRDB.

Aidha alisema kama wizara walikubaliana kują na mkakati wa kumpunguzia gharama mkulima kwenye sekta ya kilimo hivyo wameona ili kuondoa changamoto hiyo watumie chama kimoja cha ushirika.