Marekani kurejesha msaada kwa Palestina
2021-04-08 10:23:11| cri

 

 

Rais Joe Biden wa Marekani amesema nchi yake inaunga mkono kutatua suala la Palestina na Israel kwa njia ya “mpango wa nchi mbili”. Wakati huohuo wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza kuwa nchi hiyo itarejesha misaada yake kwa Palestina.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aligeuza msimamo wa muda mrefu wa nchi hiyo wa kuunga mkono “mpango wa nchi mbili”, na kupunguza msaada kwa Palestina hatua kwa hatua, na kutangaza kuwa Marekani inakubali Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.