Mafanikio ya China katika kuondokana na umaskini yaonyesha kuwa umaskini si tatizo lisiloweza kushindwa
2021-04-08 08:58:32| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amefafanua kuhusu waraka ya mafanikio ya China katika kuondokana na umaskini, akisema mafanikio hayo yanaonesha kuwa, umaskini si tatizo lisiloweza kushindwa.

Amesema njia maalumu ya kupunguza umaskini ya China imetoa mawazo na uzoefu wa kuigwa wa kutatua matatizo ya utawala katika nchi za kisasa. Ameongeza kuwa, China siku zote inatanguliza maslahi ya wananchi wake, na kutilia maanani kuondokana na umaskini, ikichukua hatua ya maendeleo kwa kuondoa umaskini, na kuhimiza mchakato wa kupambana na umaskini kulingana na hali halisi.

Amesema China inataka kuendelea kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kuhusu kupunguza umaskini pamoja na nchi mbalimbali, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa kujenga muskatabali wa maendeleo ya pamoja ya binadamu usio na umaskini.