G20 yakubali kuongeza muda wa pendekezo la kuahirisha kulipa madeni ya nchi maskini zaidi
2021-04-08 18:35:02| CRI

Mawaziri wa mambo ya fedha na wakuu wa Benki Kuu za Kundi la Nchi 20 (G20) jana wamekubali kuongeza muda wa pendekezo la kuahirisha malipo ya madeni kwa nchi maskini zaidi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2021.

Mawaziri hao pia wamelitaka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kutoa mpango wa Haki Maalum za Kutoa Fedha (SDR) wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 650, ili kusaidia kukabiliana janga la COVID-19 na kuhimiza ufufukaji wa uchumi wa dunia.

Hayo yameelezwa kwenye taarifa iliyotolewa baada ya Mkutano wa majira ya Spring wa mawaziri wa mambo ya fedha na wakuu wa Benki Kuu za nchi wanachama wa G20, na wakuu wa IMF na Benki ya Dunia.