SOKA: FIFA yaifungia Chad
2021-04-08 18:27:11| cri

Shirikisho la Soka Duniani, (FIFA) limeifungia Chad baada ya serikali ya nchi hiyo kuingilia kati namna ambavyo shirikisho la soka nchini humo linavyofanya kazi. Hatua hii imekuja baada ya Wizara ya Vijana na Michezo kuvunja Shirikisho la Soka nchini Chad mwezi Machi. Baada ya tangazo hilo lililotolewa na serikali ya Chad, Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), liliitoa timu ya taifa katika raundi ya pili ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika.