Uganda na Misri zasaini makubaliano kuhusu kubadilishana habari ili kupambana na ugaidi
2021-04-08 18:37:00| CRI

Misri na Uganda zimesaini makubaliano ya kubadilishana habari za kupambana na ugaidi katika mashariki na kaskazini mwa Afrika.

Mkuu wa Idara ya upelelezi ya jeshi la Uganda Abel Kandiho amesema makubaliano hayo yatashuhudia nchi hizo mbili zikibadilishana habari mara kwa mara, hatua ambayo ni muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Kiongozi wa ujumbe wa Misri Sameh Saber El-Degwi ambaye yuko ziarani nchini Uganda pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili.