China kutoa chanjo yake COVID-19 kusaidia mapambano dhidi ya virusi duniani kwaweka msingi wa kuihimiza iingie katika soko la kimataifa
2021-04-08 18:24:39| Cri

China kutoa chanjo yake COVID-19 kusaidia mapambano dhidi ya virusi duniani kwaweka msingi wa kuihimiza iingie katika soko la kimataifa_fororder_1126986749_16106933443171n

Chanjo ni silaha ya kupambana na virusi, pia ni matumaini ya kuokoa maisha ya watu. Wakati janga la COVID-19 linaposambaa kote duniani, China ilitangulia kuahidi kuifanya chanjo yake iwe bidhaa ya afya ya duniani, kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata chanjo hiyo kwa gharama nafuu, na kuanzisha ushirikiano wa kimataifa wa chanjo. Wataalamu wa sekta ya chanjo wameeleza kuwa, chanjo ya COVID-19 ya China itasaidia mapambano ya kimataifa dhidi ya virusi, pia itaimarisha sekta ya chanjo ya China, na kuweka msingi thabiti kwa chanjo ya China kuingia katika soko la kimataifa.

Hadi kufikia tarehe 30 Machi, China imetoa msaada wa chanjo ya virusi vya Corona kwa nchi 80 na mashirika matatu ya kimataifa, na kuuza chanjo kwa nchi zaidi ya 40 duniani. Mbali na hayo, China imejiunga na mpango wa utekelezaji wa chanjo ya COVID-19 (COVAX) chini ya Shirika la Afya Duniani (WHO), na kuahidi kutoa msaada wa shehena ya kwanza ya dozi milioni 10 ya chanjo kwa nchi zinazoendelea. China pia imekuwa ikiunga mkono viwanda vyake na wenzi wa kimataifa kufanya utafiti na uendelezaji wa pamoja, majaribio,na uzalishaji wa chanjo. Mkuu wa Shirikisho la Viwanda vya Chanjo la China Bw. Feng Duojia ameeleza kuwa, ushiriki wa chanjo ya COVID-19 ya China katika mapambano dhidi ya virusi duniani, una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya sekta ya chanjo. Anasema:

 “Hii ni mara ya kwanza kwa chanjo ya COVID-19 ya China kutumiwa kwa kiasi kikubwa katika nchi mbalimbali duniani. Pia imetoa mchango wa China kwa upatikanaji na unafuu wa chanjo katika nchi zinazoendelea duniani, pia imekuwa lengo la wazi la kwanza la kimkakati la maendeleo katika sekta ya chanjo nchini China.”

Bw. Feng amesema, hivi sasa sekta ya chanjo ya China inakabiliwa na fursa mpya za maendeleo, hali ambayo inaitaka nchi hiyo kuboresha viwanda vya chanjo, ili kuweka msingi mzuri kwa chanjo yake kuingia katika soko la kimataifa. Anasema:

“Tukitaka kuhudumia dunia nzima na kutoa bidhaa za afya ya umma duniani, ni lazima tuhakikishe sifa ya bidhaa ifikie vipimo vya kimataifa, kutoa huduma zinazolingana na kanuni za kimataifa, na kuboresha uwezo na kiwango cha uzalishaji.”

Pia ameeleza kuwa, hivi sasa Shirikisho la Viwanda vya Chanjo la China linafanya utafiti kwa kina kuhusu kuvifanya viwanda vya chanjo kuwa la kimataifa, na kukusanya maoni kutoka viwanda vinavyohusika.