TENNIS: Mashindano ya French Open yaahirishwa kutokana na COVID-19
2021-04-08 18:28:17| cri

Mashindano maarufu ya tennis ya French Open yameahirishwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ufaransa. Wizara ya Michezo nchini humo imesema serikali iliweka kizuizi cha tatu jumamosi iliyopita, ambapo rais Emmanuel Macron alisema kitamalizika katikati ya mwezi ujao, wakati mashindano hayo yalipaswa kuanza Mei 23 hadi Juni 6. Awali, mashindano hayo yalipangwa kufanyika mwaka jana, lakini yaliahirishwa hadi majira ya joto mwaka huu kutokana na janga la virusi vya Corona.