Kuganda kwa damu kunakohusishwa na chanjo ya AstraZeneca kwaorodhosheshwa kama athari ya nadra
2021-04-08 10:22:10| CRI

Kuganda kwa damu kunakohusishwa na chanjo ya AstraZeneca kwaorodhosheshwa kama athari ya nadra

 

Mamlaka ya Dawa ya Ulaya (EMA) imethibitisha kuwa matokeo ya kuganda damu yanahusiana kihalisi na chanjo ya virusi vya Corona ya AstraZeneca, lakini yanapaswa kuorodheshwa kama athari ya nadra.

Katika tathmini yake ya hivi karibuni, wataalamu wa Mamlaka hiyo wamewaambia wanahabari kuwa, matokeo ya damu kuganda ni machache, na faida kubwa ya chanjo hiyo katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona inazidi hatari la athari mbaya.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya mamlaka hiyo kuwafanyia tathmini zaidi ya watu 80 waliopata tatizo la damu kuganda katika mishipa ya damu na mishipa ya damu ya kwenye moyo baada ya kupata chanjo hiyo, ambapo watu 18 kati yao wamefariki.