Matumaini ya Uganda ya kuanza tena usafirishaji wa sukari kwenda Kenya yafifia
2021-04-08 17:09:35| cri

Matumaini ya Uganda kuanza tena mauzo ya sukari kwenda Kenya yanaendelea kufifia kutokana na Kenya kutangaza kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Wizara ya kilimo nchini Kenya imetangaza ongezeko thabiti la uzalishaji sukari kutokana na uwezekezaji ulioimarishwa na wadau wa serikali na sekta binafsi ikigundulika kuwa mnamo mwaka 2020 pekee uwezo wa sekta ya sukari ulikua hadi tani 603,788 ikilinganishwa na tani 440,935 mwaka 2019,na kusababisha ongezeko la asilimin 37 la uzalishaji wa ndani.

Uganda ilikuwa na matumaini ya kurejelea usafirishaji wa sukari kwa moja ya washirika wake wakuu wa kibiashara lakini viashiria vinaonyesha kuwa Kenya imeongeza uzalishaji wa sukari.

Mwenyekiti wa Chama cha Watengezaji Sukari cha Ugand,Bw Jim Kabeho jana alisema hawajui kinachoendelea kwa sababu Kenya imewaeka gizani kuhusiana na mchakato utakaopelekea kuanza tena mauzo ya nje.