Biashara ya China yaonyesha mwelekeo mzuri katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu
2021-04-08 20:08:30| CRI

Biashara ya China yaonyesha mwelekeo mzuri katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu_fororder_VCG111312976882

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Bw. Gao Feng leo amesema, biashara ya nje ya China imeonyesha mwelekeo mzuri katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.

Bw.Gao amesema, hojaji iliyofanywa na wizara hiyo kwa kampuni ya biashara ya nje zaidi elfu 20 za China, oda zao zimeongezeka zikilinganishwa na mwaka jana. Amesema wizara hiyo itafuatilia kwa karibu maendeleo ya hali ya kimataifa, kudumisha utulivu na uendelevu wa sera ya China, kuboresha sera za biashara, na kuendelea kuzisaidia kampuni katika kupunguza gharama na kuongeza ufanisi. Pia kufanya jitihada zote katika maendeleo madhubuti ya uuzaji na uagizaji bidhaa, na kuhimiza biashara ya nje ya China kuendelezwa kwa utulivu na kuongeza sifa.