Mkutano wa mawaziri wa G20 watoa wito wa kuendelea kutoa fedha ili kukabiliana na COVID-19
2021-04-08 08:57:27| cri

 

 

Mawaziri wa fedha na wakurugenzi wa Benki Kuu za nchi wanachama wa Kundi la Nchi 20 (G20) wamekubaliana kuhusu kuendelea kuziunga mkono kifedha nchi zinazopambana na janga la COVID-19 “kwa muda mrefu kama zinavyohitaji”.

Waziri wa uchumi na fedha wa Italia Bw. Daniele Franco amesema, kukabiliana na uharibifu wa uchumi kutokana na COVID-19 ni kipaumbele cha Kundi hilo. Ameongeza kuwa washiriki wa mkutano wa pili wa kundi hilo wamekubaliana kutumia “vyombo vyote vya sera kwa muda mrefu kama inavyohitajiwa” ili kuokoa maisha na ajira.

Bw. Franco pia amesema, kuongeza utoaji wa chanjo ya COVID-19 duniani kwa njia ya usawa na inayopatikana ni sehemu ya juhudi hizo.