Watu 8,000 wauawa na mabomu ya kutegwa ardhini nchini Yemen
2021-04-08 10:24:51| cri

 

 

Watu zaidi ya 8,000 wameuawa kwa mabomu yaliyotegwa ardhini na kundi la Houthi wakati wa vita vya ndani nchini Yemen. Shirika la habari la serikali la Yemen Saba limesema, tangu kuanza kwa vita mnamo Septemba mwaka 2014, mabomu hayo yamesababisha maafa makubwa ya kibinadamu nchini Yemen, na kati ya watu waliouawa ni pamoja na watoto na wanawake.

Ripoti zilizotolewa na mashirika ya kibinadamu zinasema, tangu Vita Vikuu vya Pili duniani, Yemen imekuwa moja ya nchi ambazo mabomu mengi ya ardhini yametegwa .