Mkurugenzi wa elimu acheza Breaking dansi kwa ajili ya wanafunzi
2021-04-14 17:06:24| Cri

Hivi karibuni video moja inayoonesha mwanume akicheza Breaking dansi kwenye jukwaa na kushangiliwa sana na wanafunzi wake, imesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanaume huyo ni mkurugenzi wa idara ya elimu ya wilaya ya Jianwei mkoani Sichuan Bw. Duan Fuli. Siku hiyo baada ya kutoa hotuba kwa wanafunzi katika shule moja ya sekondari ya juu, alianza kucheza dansi jukwaani ili kuwaburudisha wanafunzi wa mwaka wa mwisho watakaoshiriki kwenye Mtihani wa Taifa wa Kujiunga na Vyuo Vikuu.

Wanamtandao wengi walibofya “Like” kwenye video hiyo na kusema mkurugenzi huyo alicheza dansi vizuri sana, na kuona njia hii inasaidia kuwapunguzia wanafunzi mfadhaiko unaotokana na mtihani.