Maonyesho ya Canton yaanza kwa kupitia mtandaoni
2021-04-15 19:10:42| Cri

Maonyesho ya Canton yaanza kwa kupitia mtandaoni_fororder_1183896684316852238

Maonyesho ya 129 ya Uagizaji na Uingizaji Bidhaa ya China yanayojulikana kama Maonyesho ya Canton, yameanza leo kwa njia ya mtandao huku bidhaa nyingi zikionyeshwa.

Msemaji wa maonyesho hayo, Xu Bing amesema, kampuni zinazoshiriki maonyesho hayo zimewasilisha zaidi ya bidhaa milioni 2.7, ambazo ni 230,000 zaidi ya maonyesho yaliyopita, na kuongeza kuwa, mabanda 60,000 yameandaliwa kwa ajili ya washiriki 26,000 wa ndani na nje ya nchi.

Maonyesho hayo ya siku kumi yataendelea hadi tarehe 24 mwezi huu, na ni mara ya tatu kwa maonyesho hayo kufanyika kwa njia ya mtandao, kufuatia maonyesho yaliyofanyika mwezi Juni na Oktoba mwaka jana.