GDP ya China yaongezeka kwa asilimia 18.3 kuliko mwaka jana wakati kama huu
2021-04-16 18:44:43| CRI

GDP ya China yaongezeka kwa asilimia 18.3 kuliko mwaka jana wakati kama huu_fororder_VCG111325925840

Msemaji wa Idara ya takwimu ya China Bibi Liu Aihuai, amesema katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, uchumi wa China umeendelea kwa utulivu, pato la taifa GDP limeongezeka kwa asilimia 18.3 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

Bibi Liu amesema mahitaji ya uzalishaji yameboreshwa, hali ya ajira na bei ya bidhaa zimekuwa na utulivu, motisha mpya wa uchumi umongezeka kwa kasi, sifa na ufanisi umeinuka kwa hatua madhubuti, na matarajio ya soko yana mwelekeo mzuri. Kutokana na pande hizo tano, uchumi wa China katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu umeendelea na hali ya kufufuka.