Sheria ya China ya kudhibiti uvutaji wa tumbaku yawalinda karibu asilimia 12 ya watu
2021-04-21 12:44:01| Cri

Hivi karibuni Kituo Kipya cha Utafiti wa Maendeleo ya Afya kilitoa ripoti kuhusu hali ya udhibiti wa uvutaji wa tumbaku ya China ya mwaka 2020.

Ripoti hiyo imesema, uvutaji wa sigara na moshi wa sigara kwa njia zisizo moja kwa moja, ni chanzo muhimu cha magonjwa mbalimbali sugu. Matokeo ya utafiti yaliyotolewa hivi karibuni kuhusu magonjwa ya dunia yameonesha kuwa, kila mwaka idadi ya watu nchini China wanaofariki kutokana na uvutaji wa sigara au moshi wa sigara kwa njia zisizo moja kwa moja imezidi milioni 1, na sheria na kanuni za kudhibiti sigara zimewalinda asilimia 12 ya watu, hata hivyo bado kuna pengo kubwa kwa sheria hiyo kufikia lengo la kuwahusisha asilimia 30 ya watu ifikapo mwaka 2022.

Ripoti hiyo inatoa wito wa kuongeza nguvu katika kudhibiti uvutaji wa sigara na hatua ya kujenga mazingira yasiyo na sigara, na kuzingatia umuhimu wa kudhibiti matumizi ya sigara kwa vijana.