WHO yasema watoto laki6.5 kwenye nchi 3 za Afrika wapatiwa chanjo ya ugonjwa wa Malaria
2021-04-21 09:09:50| CRI

Shirika la afya duniani WHO limesema zaidi ya watoto laki 6.5 nchini Ghana, Kenya na Malawi wamepatiwa chanjo ya ugonjwa wa malaria katika kipindi cha miaka miwili iliyopita tangu mpango wa kutoa chanjo hiyo uanze.

Mkurugenzi wa Idara ya kinga, chanjo na mambo ya kibiolojia wa WHO Bibi Kate O’Brien, amesema nchi hizo tatu zimeweka miundo mbinu imara kuhakikisha watoto wanapewa chanjo hiyo.

Zaidi ya dozi milioni 1.7 za chanjo ya kwanza dhidi ya ugonjwa wa Malaria imetolewa kwenye kipindi cha majaribio katika nchi hizo tatu kwenye mpango ulioanza mwaka 2019. WHO imesema data zitakazopatikana kwenye majaribio hayo, zitaangalia uwezekano wa kutumiwa kwa chanjo hiyo kwenye eneo kubwa zaidi.