Benki yamrudishia mzee pesa alizohifadhi benkini baada kufariki kwake
2021-04-21 12:35:28| Cri

Miaka 11 iliyopita Bibi mzee mmoja wa mkoa wa Hubei aliweka benkini RMB yuan laki 6.5, sawa na dola za kimarekani laki moja kwa muda wa mwaka mmoja na hakuzichukua baada ya hapo.

Hivi karibuni wafanyakazi wa benki waliwasiliana na binti wa mzee huyo na kujua kuwa mzee alikuwa amekufa, na hata binti huyo hakujua kuhusu uwepo wa pesa hizo. Bintihiyo alikumbwa na mshangao. Pengine mzee huyo alihifadhi pesa kwa muda mrefu sana, kwa hivyo alisahau kumwambia binti yake kuhusu jambo hilo. Kwa bahati benki ilimjulisha kwa wakati, la sivyo pesa zingepotea.

Watu wengi wanasifu kitendo hicho cha benki, wakiona kuwa ingawa benki ina jukumu la kutunza mali za wateja, lakini kama mteja hakuchukua pesa, benki inaweza kuziacha bila kuzishughulikia, na pesa hizo zitawekwa benkini daima na hakuna mtu atakayejua. Wengine wanatumai kuwa benki inaweza kufuatilia akaunti za wazee, na kuwaarifu jamaa wa wateja kama hao. Ikiwa baadhi ya wazee hawapendi kuchukua pesa hizo, ni chaguo zuri kwa kuichia jamii.