Tarehe 22 usiku kwa saa za Beijing, mkutano wa kilele kuhusu mabadiliko ya tabianchi umefanyika, ambapo rais Xi Jinping wa China ameshiriki kwa njia ya video na kuhutubia mkutano huo kutoka hapa Beijing.
Rais Xi amesisitiza kuwa, ili kukabiliana na matatizo makubwa ambayo hayajawahi kutokea zamani katika usimamizi wa mazingira duniani, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa na nia na hatua thabiti, kuwajibika na kushirikiana kwa mshikamano, na kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu na viumbe vingine.
Tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza ajenda ya mkutano huo wa siku mbili, ambao utajadili kuinua nia ya kukabiliana mabadiliko ya tabianchi, uwezo na unyumbufu wa kuzoea mabadiliko hayo, usalama wa hali ya hewa, teknolojia yenye uvumbuzi ya kukabiliana mabadiliko ya tabianchi, na fursa ya kiuchumi inayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.