Russia yahimiza ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2021-04-23 08:39:52| CRI

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema nchi yake inapendekeza kuongeza ushirikiano wa kimataifa katika kutafuta ufumbuzi wenye ufanisi kwa suala la mabadiliko ya tabianchi duniani.

Akihutubia katika Mkutano wa Kilele Kuhusu Tabianchi kwa njia ya video, Rais Putin amesema mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi yanahitaji juhudi za pamoja za jumuiya ya kimataifa, na kwamba makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa yanaweka msingi imara wa kisheria kwa ushirikiano wa kimataifa wa kudhibiti na kupunguza utoaji wa hewa ukaa.