Biden kuhudhuria mkutano wa kilele wa NATO mwezi Juni
2021-04-23 20:05:31| CRI

Habari kutoka Shirika la Habari la Marekani AP zinasema rais Joe Biden wa Marekani atahudhuria mkutano wa kilele wa NATO utakaofanyika mjini Brussels tarehe 14 Juni.

Habari zinasema mkutano huo utakuwa wa ana kwa ana, na utakuwa ni fursa ya kupunguza hali ya wasiwasi kati ya Marekani, Ulaya na Canada iliyosababishwa na aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump.

Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg imesema mkutano huo utajadili “changamoto za usalama za siku hizi na siku za baadaye: operesheni ya uvamizi ya Russia, tishio la ugaidi, mashambulizi kwenye mtandao wa Internet, teknolojia mpya na zenye madhara, athari ya mabadiliko ya tabianchi kwa usalama, na ustawi wa China”.